Thursday 13 March 2014

Picha za Ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Kitaifa Jijini Tanga

 
 Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mlaji, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Mohammed Chima, akisaini kitabu cha wageni katika banda la SUMATRA, huku Afisa Habari wa SUMATRA, Maria Mselem (wa pili kushoto) alipotembelea banda la mamlaka hiyo jijini Tanga, leo Machi 13, 2014.


Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Mlaji, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Mohammed Chima, akipokea vipeperushi kuhusu shughuli za Tume ya Ushindani kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Tume hiyo, Frank Mdimi, alipotembelea banda la Tume jijini Tanga, leo Machi 13, 2014.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Mohammed Chima, akisikiliza maelezo ya shughuli za Baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Shughuli zinazodhibitiwa wa SUMATRA kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Oscar Kikoyo (wa tatu kushoto kwa Bw, Chima), alipotembelea banda hilo  jijini Tanga, Machi 13, 2014. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri kwa Watumiaji wa Huduma za TCAA, Bw. Juma Fimbo, ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Walaji (TCF) walioandaa maonesho hayo.
Wawakilishi kutoka Mabaraza ya Ushauri kwa Walaji, Mamlaka za Udhibiti, FCC na Vyuo na shule zilizoshiriki katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mlaji kitaifa, wakiwa na mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Mohammed Chima, wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Mlaji, jijini Tanga, leo, Machi 13, 2014.

Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mlaji Kitaifa Jijini Tanga, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Mohammed Chima, akihutubia wakati akifungua maadhimisho hayo leo, Machi 13, 2014.
 Wawakilishi wa asasi zinazoshiriki maonesho ya Siku ya Haki za Mlaji jijini Tanga wakiwa na mgeni Rasmi katika picha ya pamoja leo, Machi 13, 2014.

No comments:

Post a Comment