Tuesday 25 March 2014

Mdahalo wa Wazi Wapamba Maadhimisho ya Haki za Mlaji Tanga

Mdahalo wa wazi umekuwa kivutio kikubwa katika maadhimisho ya kitaifa ya Haki za Mlaji Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Tropikana,Mabawa, Jijini Tanga. Mdahalo huo uliofanyika siku ya ufunguzi wa maadhimisho hayo, tarehe 13 Machi, 2014, ulihusisha shule na vyuo kadhaa zikiwemo Chuo Kikuu cha Eckenforde, Chuo cha ualimu cha Eckenforde, Shule ya Sekondari ya Popatlal, Chuo cha Biashara cha Mtakatifu Joseph na Shule ya Sekondari ya Usagara.

Wanafunzi hao walionekana kuelewa vema shughuli za mabaraza ya ushauri kwa walaji ya mamlaka za udhibiti lakini wengi wao walijikita katika kujadili masuala yanayohusu usafiri wa abiria mijini (Daladala) na usafiri wa mwisho wa mwaka wa mabasi ya abiria baina ya mikoa.

No comments:

Post a Comment