FCC Yakamata Bidhaa Bandia
za Sh. Mil 30/- Mwanza na Arusha
Wakaguzi
wa Tume ya Ushindani (FCC), wakifanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya Alama za
Bidhaa (1963), iliyorekebishwa, pamoja na kanuni za Sheria hiyo za mwaka 2012,
wameendesha zoezi la kaguzi za kushitukiza katika miji ya Arusha na Mwanza kati
ya Aprili 8 na 12 na kukamata bidhaa bandia zenye thamani ya Sh. Milioni 30/-.
Bidhaa
zilizokamatwa katika kaguzi za kushitukiza jiini Mwanza ni kama ilivyoainishwa
hapa chini:
Na.
|
Duka/Mmiliki
|
Bidhaa Bandia Zilizokamatwa
|
Eneo
|
1
|
M/S Shaban Hussein Kombe (S.K Mobile Phone Shop)
|
Simu bandia aina
ya Tecno mobile (216pcs) na
betri zake (2,556)
|
Mtaa wa Msikiti Wa
Ijumaa
|
2
|
Duka la M/S Yassin Ibrahim Nyaludibha
|
Baygon (12pcs)
|
Mtaa wa Liberty
|
3
|
M/S Mama Mwijage Mini Super Market
|
Baygon (1pc) na kiwi
(1pc)
|
Mtaa wa Liberty
|
4
|
Duka la Patric
|
Baygon (1pc)
|
Mtaa wa Liberty
|
5
|
M/S Sammiyya Najib Zaharo Mini Super Market
|
Baygon (1pc)
|
Mtaa wa Liberty
|
Operesheni
iliyofanyika jijini Mwanza ilihusisha pia ukamataji wa bidhaa bandia za
vipodozi 494 vilivyopigwa marufuku. Bidhaa hizo zilikabidhiwa kwa mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Vipodozi hivyo ni pamoja na Carolight
(190pcs), Losheni ya Betasol na krimu yake ya carl (188), Krimu ya Diproson (20
pcs) Losheni ya Diproson (12 pcs), Cocoderm (18 pcs) na Prolight (18 pcs). Vipodozi vyote vilipatikana katika duka
la Bw. Yassin Ibrahim Nyaludibha.
Maduka
mengine ambayo yalikaguliwa lakini hayakukutwa na bidhaa bandia ni pamoja na Iman
Shop, Lake Printing Works Ltd., Sahara Shop, George
Mwendeshe Lukoninga, Joyce Kwandu Kichiba, Emmanuel Joseph Sisha, Abogast Marko
Mhalagani, Aron Kisasa Shop na Dunia Mashala Ng’wanaomu.
Aidha,
operesheni ya kaguzi zilizoendeshwa jijini Arusha pia iliwezesha kukamatwa kwa
bidhaa bandia kama ilivyoainishwa hapa chini:
Na.
|
Duka/Mmiliki
|
Bidhaa Bandia Zilizokamatwa
|
Eneo
|
1
|
Highland Hardware
|
Lorenzetti heater 1pc
|
Mtaa wa Sokoine
|
2
|
Baltazari Mallya
|
Lorenzetti heater 3pcs
|
Mtaa wa Sokoine
|
3
|
CBK
trading
|
Lorenzetti heater 40pcs
|
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
|
4
|
Angelika Quality store
|
Lorenzetti heater 2pcs
|
Mtaa wa Levolusi
|
5
|
Maria Inocent Massawe
|
Losheni za Nivea (1pc)
|
|
6
|
Baraka Mangaro Nkya
|
Losheni za Nivea (11pcs)
|
Mtaa wa Annex
|
7
|
Shamika Enterprises
|
Losheni za Nivea (28pcs)
|
Mtaa wa Kaloleni
|
8
|
Super Cosmetics
|
Losheni za Nivea (56 pcs)
|
|
9
|
Janet Cosmetics
|
Losheni za Nivea (34 pcs)
|
|
10
|
Felix O Kimario
|
Mafuta ya kulainisha midomo ya Nivea (lip shine)
(5 pcs)
|
Mtaa wa Levolosi
|
11
|
Raymond Cosmetics
|
Losheni za Nivea (28pcs)
|
Mtaa wa Zaramo
|
Karibu
watuhumiwa wote walitimiza masharti ya utaratibu wa Mkondo wa haraka wa
utanzuaji mashauri kwa mujibu wa Sheria ya Alama za Bidhaa (offence
compoundment procedure) na kulipa faini kwa mujibu wa taratibu na kanuni za
sheria hiyo, wakati bidhaa walizokamatwa nazo zikisubiri kuteketezwa.
Hata
hivyo, mtuhumiwa mmoja, M/S Shamika Enterprises, alieleza dhamira yake ya
kutumia mkondo wa mahakama za kawaida kupinga utaratibu wa adhabu uliotumiwa na
Mkaguzi Mkuu wa MMA katika kumuadhibu. Shauri hilo litafuata Mkondo wa Sheria
ya Makosa ya jinai kama ilivyoainishwa katika Sheria husika.
Kaguzi
zote ziliendeshwa kwa kushirikiana na wasimamizi na wawakilishi wa wamiliki wa
hataza na miliki bunifu zilizobainika kughushiwa katika bidhaa zilizokamatwa,
pamoja na maafisa wa jeshi la polisi.
Wakaguzi
wa FCC pia waliendesha kaguzi katika maduka manne ya mauzo ya jumla na reja
reja ya betri za Tiger Head mnano tarehe 9 Aprili, 2014. Maduka hayo ni pamoja
na Neema Investment, Duka la Nancy, Duka la Mtei, na duka la Setway pamoja na
maghala yanliyoshukiwa kuhusiana na maduka hayo katika maeneo ya Unga Limited,
Moromboo na Mbauda. Maduka na ghala hizo hayakukutwa na bidhaa bandia za Tiger
Head zilizohofiwa kuhodhiwa humo.
Hatua
hiyo ni mwendelezo wa juhudi za Tume zilizofanywa na tume za kufanya kaguzi za
kawaida pamoja na kaguzi nyingine 7 za kushitukiza katika maduka na bohari
zinazomilikiwa na watu binafsi, ambazo zinahofiwa kuhodhi bidhaa bandia, baina
ya Julai 1, 2013 na Aprili 11, 2014 katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam. Operesheni
hizo ziliwezesha kukamatwa kwa bidhaa bandia ikiwa ni pamoja na makontena 240
yaliyokuwa na shehena za bidhaa bandia zenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni
200/- na wafanyabiashara wapatao a71 kuadhibiwa kwa kukiuka Sheria ya Alama za
Bidhaa. Baadhi ya bidhaa zilizokamatwa katika operesheni hizo za awali ni
pamoja na Simu bandia za Samsung, NOKIA and TECNO zaidi ya 400, Mabomba 738 ya maji
ya IPS, Vifaa vya michezo 1,248
vya Klabu ya Mpira ya Simba, Vyandarua za kuzuia mbu, Vifaa 1,166 vya umeme vya
Phillips, Pakiti 12,053 za nyembe bandia za Gillette na Swichi za Umeme aina ya
MEM zipatazo 19.
Operesheni
za kaguzi za kushitukiza katika maeneo yote yanayohofiwa kuhodhi bidhaa bandia
ni zoezi endelevu na linaendeshwa kote nchini likilenga kuwakamata na
kuwafikisha katika mkono wa sheria wahalifu wote wanaojishughulisha na biashara
ya bidhaa bandia. Kusjishughulisha na biashara ya bidhaa bandia kunawaathiri wamiliki
hataza na miliki bunifu, kuaathiri uchumi na kunakiuka haki za walaji nchini.
Imetolewa
na Mkaguzi Mkuu wa Sheria ya Alama za Bidhaa
MKAGUZI
MKUU, SHERIA YA ALAMA ZA BIDHAA
Aprili 22, 2014
No comments:
Post a Comment