Thursday 31 August 2017

FCC Yakamata Bidhaa Bandia za Thamani ya TZS 441,355,530/-

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

FCC Yakamata Bidhaa Bandia za Thamani ya 
TZS 441,355,530/-

DAR ES SALAAM, Agosti 30, 2017. Tume ya Ushindani, ikifanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya Alama za Bidhaa ya mwaka 1963, iliyorekebishwa, imefanya kaguzi za kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Mtwara na kukamata bidhaa bandia zenye thamani ya TZS 441,355,530/- kati ya Januari na Julai, 2017. Bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na:

1.   Spika 59 za muziki zilizokuwa na nembo ya kughushi ya FIDEK, zenye thamani ya TZS TZS 53,100,000/-,
2.   Spika 30 za muziki zilizokuwa na nembo ya kughushi ya Crown, zenye thamani ya TZS 15,000,000/-,
3.   Kofia ngumu za waendesha pikipiki 1,246 zilizokuwa na nembo ya kughushi ya FEKON zinazokadiriwa kuwa na thaman ya TZS 18,640,000/=
4.   Pikipiki nane (8) zilizokuwa na nembo ya kughushi ya SANLG pamoja na injini 7 za pikipiki, vyote vikiwa na thamani ya TZS 19,400,000/-
5.   Vijiko vitatu vya kubebea mizigo vilivyokuwa na nembo ya kughushi ya HELI na vyenye thamani ya TZS 167,607,765/-
6.   Jozi 5,889 za viatu zilizokuwa na nembo ya kughushi ya PUMA, zenye thamani ya TZS 235,560,000/-.

Mazoezi yote ya kaguzi za kushitukiza yaliyotokana na taarifa za ukaguzi wa masoko na uchunguzi wa bidhaa bandia katka soko.

Wafanyabiashara waliokamatwa na bidhaa hizo bandia wapo katika hatua mbalimbali za kukamilisha matakwa ya sheria kuhusiana na adhabu walizopewa baada ya kukutwa na bidhaa hizo, kama ilivyoainishw akatika Sheria ya Alama za Bidhaa (183), iliyorekebishwa pamoja na kanuni zake.

FCC inawaasa wauzaji jumla na rejareja wa bidhaa zote kujiepusha na biashara ya bidhaa bandia kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai linaoadhibiwa kwa faini na vifungo hela.

BIashara ya bidhaa bandia husababisha ushindani usio haki sokoni kwa na unawakimbiza na kuwaogopesa wawekezaji wa viwanda kuanzisha shughuli zao hapa nchini.

Walaji pia wanaaswa kukagua bidhaa wanazozinunua sokoni kabla ya kuzilipia. Wanatakiwa kugaua ukamilifu wa bidhaa, maelezo ya bidhaa  ikiwa ni pamoja na anuani ya mtengenezaji, nchi ya uasili, maelezo ya matumizi, vyeti vya uthibitiho wa ubora wa bidhaa kutoka kwa mtengenezaji. Aidha, walaji wana wajibu wa kudai risiti stahiki kw akila manunuzi waliyoyafanya. Pia wanatakiwa kutoa taarifa za matukio ya ukiukwaji wa haki na maslahi yao katika Tume na vyombo vingine.

Ofisi za FCC zipo Ghorofa ya pili ya jengo la GEPF, Barabara ya Bagamoyo, simu namba +255 22 2926128/29/30.

Kaguzi za kushitukiza katika maeneo binafsi ya kibiashara pamoja na kaguzi za kila siku katika maeneo ambayo ni maingilio ya bidhaa (bandarini na bandari kavu) ni mazoezi endelevu, Wafanyabiashara wote wanatakiwa kutii matakwa ya sheria ya alama za bidhaa bila shuruti.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Frank S. Mdimi, Afisa Mwandamizi, Mawasiliano na Mahusiano ya Umma, Tume ya Ushindani, Simu ya Kiganjani +255-784762437, Barua Pepe: fmdimi@competition.or.tz

No comments:

Post a Comment