Wednesday 6 September 2017

Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC, Akutana na Wafanyakazi

Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC Akutana na Kuzungumza na Wafanyakazi 

DAR ES SALAAM, Septemba 5, 2017. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dk. John Kedi Mduma, amefanya mikutano na Kurugenzi zote za Tume ya Ushindani ili kujifunza kuhusu shughuli za Kurugenzi hizo na idara zilizo chini ya Kurugenzi hizo na kujua shughuli wanazozifanya, mafanikio na changamo wanazokabiliana mazo.

Kurugenzi zilizohusika na vikao hivyo ni pamoja na Kurugenzi ya Miungano ya Kampuni, Utafiti na Utetezi wa Ushindani, inayoongozwa na Dk. Allan S. Mlulla, Kurugenzi ya Kushughulikia Makosa Yanayodhiisha Ushindani, inayoongozwa na Dk. Deo Nangela, Kurugenzi ya Utetezi wa Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia inayoongozwa na Godfrey Gabriel.

Kurugenzi hizo zilielezea shughuli zake zilizopo katika mpango kazi, vipaumbele, changamoto na namna wanavyokabiliana nazo.


Katika mikutano hiyo, majadiliano ya namna ya kuboresha utendaji pia yalifanyika.

Kaimu Mkurugenzi huyo alitambulishwa kwa wafanyakazi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Vianda, Biashara na Uwekezaji (anayeshughulikia biashara na uwekezaji), Profesa Adolph Mkenda, siku alipoanza kazi rasmi kushika wadhifa huo, tarehe 28 Agosti, 2017.

No comments:

Post a Comment