Wednesday 20 September 2017

FCC Katika Channel Ten Alhamisi Septemba 21, 2017

Usikose mahojiano maalum katika Channel Ten tarehe 21 Septemba, 2017 kuanzia saa nne kamili hadi nne na nusu usiku. Maimu Mkurugenzi Mkuu, Dk. John Kedi Mduma, Kaimu Mkurugenzi wa Utetezi wa Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia, Godfrey Gabriel, Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia, Zaytun Kikula na Afisa Mkaguzi wa Bidhaa Bandia, Mike kajembe, watashiriki katika mahojiano yatakayooendeshwa na Mtangazaji Donald Mtani.
 
USIKOSE.



Wednesday 6 September 2017

Picha za Vikao vya Kurugenzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC

   Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bibi Anne Mbughuni, akimweleza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume, Dk. John Kedi Mduma (kushoto), kuhusu shughuli za kurugenzi yakı katika ukumbi wa mikutano wa Tume, Septemba 5, 2017.

   Wafanyakazi wa Kurugenzi ya Uendeshaji wakifuatilia wasilisho la Kaimu Mkurugenzi wao, Bibi Anna Mbughuni katika kikao na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dk. John Kedi Mduma katika ukumbi wa mikutano wa Tume, Septemba 5, 2017.

    Wafanyakazi wa Kurugenzi ya Uendeshaji wakifuatilia wasilisho la Kaimu Mkurugenzi wao, Bibi Anna Mbughuni katika kikao na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dk. John Kedi Mduma katika ukumbi wa mikutano wa Tume, Septemba 5, 2017.

   Wafanyakazi wa Kurugenzi ya Utetezi wa Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia wakifuatilia wasilisho la Kaimu Mkurugenzi wao, Bw. Godfrey Gabriel katika kikao na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dk. John Kedi Mduma katika ukumbi wa mikutano wa Tume, Septemba 5, 2017.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC, Akutana na Wafanyakazi

Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC Akutana na Kuzungumza na Wafanyakazi 

DAR ES SALAAM, Septemba 5, 2017. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dk. John Kedi Mduma, amefanya mikutano na Kurugenzi zote za Tume ya Ushindani ili kujifunza kuhusu shughuli za Kurugenzi hizo na idara zilizo chini ya Kurugenzi hizo na kujua shughuli wanazozifanya, mafanikio na changamo wanazokabiliana mazo.

Kurugenzi zilizohusika na vikao hivyo ni pamoja na Kurugenzi ya Miungano ya Kampuni, Utafiti na Utetezi wa Ushindani, inayoongozwa na Dk. Allan S. Mlulla, Kurugenzi ya Kushughulikia Makosa Yanayodhiisha Ushindani, inayoongozwa na Dk. Deo Nangela, Kurugenzi ya Utetezi wa Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia inayoongozwa na Godfrey Gabriel.

Kurugenzi hizo zilielezea shughuli zake zilizopo katika mpango kazi, vipaumbele, changamoto na namna wanavyokabiliana nazo.


Katika mikutano hiyo, majadiliano ya namna ya kuboresha utendaji pia yalifanyika.

Kaimu Mkurugenzi huyo alitambulishwa kwa wafanyakazi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Vianda, Biashara na Uwekezaji (anayeshughulikia biashara na uwekezaji), Profesa Adolph Mkenda, siku alipoanza kazi rasmi kushika wadhifa huo, tarehe 28 Agosti, 2017.

Monday 4 September 2017

Toa Taarifa Unapokutana na mikataba inayomkandamiza mlaji

Wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiweka mikataba inayokwepa uwajibikaji na kumkandamiza mlaji. Kuanzia Januari 1, 2016, Tume imeanza kupokea, kupitia na kusajili mikataba ya mlaji inayoandaliwa na mto huduma kwa nia ya kuonda vipengele vinavyokwepa uwajibikaji na kumkandamiza mlaji. Unapokuwa katika shughuli za kupata huduma ukakutana na mikataba ya huduma kwa mlaji ya aina hii, wasiliana na Tume ya Ushindani kwa Namba ya simu 22 2926128-31. Barua pepe info@competition.or.tz