Tume ya Ushindani ni moingoni mwa
Taasisi, Idara za Serikali Wakala
na Wizara zitakazoshiriki katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka
2014.
Kurugenzi zote za Tume ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Kurugenzi ya Uendeshaji; Kurugenzi ya Tafiti za Kiuchumi, Ushawishi wa Ushindani na Miungano ya Kampuni; Kurugenzi ya Utekelezaji wa Sheria na Kurugenzi ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia na Utetezi wa Mlaji, zitawakilishwa katika maonesho hayo.
Kurugenzi zote za Tume ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Kurugenzi ya Uendeshaji; Kurugenzi ya Tafiti za Kiuchumi, Ushawishi wa Ushindani na Miungano ya Kampuni; Kurugenzi ya Utekelezaji wa Sheria na Kurugenzi ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia na Utetezi wa Mlaji, zitawakilishwa katika maonesho hayo.
Katika maonesho hayo, Tume
inatarajia kuonesha shughuli zake inazozifanya kwa mujibu wa sheria
inazosimamia utekelezaji wake ambazo ni Sheria ya Ushindani (Namba 8 ya mwaka 2003) na
Sheria ya Alama za Bidhaa ya mwaka 1963, kama ilivyorekebishwa.
Kwa upande wa Sheria ya
Ushindani, Tume inatarajia kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ambavyo inashughulikia
masuala ya mashauri au kesi zinazohusu ukiukwaji wa misingi na sheria ya
ushindani, pamoja na masuala ya utetezi wa Mlaji.
Aidha, Tume itaelezea kuhusu
mikakati ya udhibiti wa Bidhaa Bandia kupitia Sheria ya Alama za Bidhaa ya mwa a1963, iliyorekebishwa, ikiwa
ni pamoja na misako mbalimbali inayofanywa na Tume katika kudhibiti bidhaa Bandia
nchini, kaguzi za kila siku katika maingilio ya bidhaa, hususan bandari na
bandari kavu zake.
Pamoj na hayo, tume pia
imejipanga kusambaza vipeperushi mbalimbali vitakavyotoa elimu kwa umma kama
vile Ijue Tume ya Ushindani, Jinsi ya Kutambua Bidhaa Bandia pamoja na
kipeperushi cha Haki na Wajibu wa Mlaji.
Mbali ya Vipeperushi hivyo, Tume
pia itatoa elimu kwa vitendo kuhusu jinsi ya kutambua bidhaa bandia kwa wananch
watakaotembelea banda lake.
Utambuzi wa viashiria vya msingi vya bidhaa bandia ni suala muhimu kwa mlaji awapo sokoni kwa kuwa litasaidia kumuwezesha kutilia mashaka bidhaa husika na kuikagua zaidi kabla ya kufanya uamuzi wa kuinunua
Aidha, ili kujipanga katika
kuboresha shughuli zake hapo baadaye, hususan katika eneo la utoaji elimu kwa
umma, Tume inatarajia kuendesha zoezi la kukusanya maoni ya wananchi kuhusiana
na namna wanavyopenda shughuli za Tume ziboreshwe na namna ambavyo kwa sasa
wanakabiliana na changamoto mbalimbalil kimaisha zinazohusiana kwa namna fulani
na shughuli za Tume; Mathalan, weledi na changamoto katika manunuzi ya bidhaa
na huduma wawapo sokoni.
Banda la Tume ya Ushindani (FCC) lipo
mstari wa kwanza, nyuma ya mabanda yaliyo mstari wa mbele unapoingia katika
lango kuu la Viwanja vya Mnazi Mmoja. Banda lipo upande wa kulia ukiingia lango
Kuu la viwanja hivyo.
Tunawakaribisha wadau wote kutembelea Banda la Tume ya Ushindani (FCC) Katika Maonesho ya WIki ya Utumishi wa Umma (2014) na kujifunza kuhusu shughuli za Tume. Katika banda hilo utaweza kupata
maelezo mbalimbali kuhusu shughuli za FCC.
No comments:
Post a Comment