Wednesday 18 June 2014

FCC Katika Maonesho ya Utumishi wa Umma

Waandaaji wa Banda la FCC wakiendelea maandalizi ya banda katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Juni 15, 2014 kwa ajili ya Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Waandaaji wa Banda la FCC wakiendelea maandalizi ya banda katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Juni 15, 2014 kwa ajili ya Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Maafisa wa FCC wakihudumia wananchi katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 16, 2014.
Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano wa FCC, Bw. Frank Mdimi, akiwaeleza wananchi kuhusu shughuli za Tume katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 16, 2014.

Afisa Mkaguzi wa Bidaa Bandia wa FCC, Mgasi Kalindimya (kushoto)  akimhudumia mwananchi katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 16, 2014.
Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano wa FCC, Bw. Frank Mdimi, akiwaeleza wananchi kuhusu shughuli za Tume katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 16, 2014.

Afisa Mkaguzi wa Bidaa Bandia, Mgasi Kalindimya wa FCC akiwahudumia mwananchi katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 17, 2014.
Afisa Mkaguzi wa Bidaa Bandia, Mgasi Kalindimya (kushoto) wa FCC akimhudumia mwananchi katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 17, 2014.
Afisa Mkaguzi wa Bidaa Bandia, Mgasi Kalindimya (kushoto) wa FCC akimhudumia mwananchi katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 16, 2014.
Afisa Mkaguzi wa Bidaa Bandia, Mgasi Kalindimya (kushoto) wa FCC akimhudumia mwananchi katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 17, 2014.
Afisa Mkaguzi wa Bidaa Bandia, Mgasi Kalindimya (kushoto) wa FCC wakihudumia wananchi katika Banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Juni 17, 2014.



Sunday 15 June 2014

FCC Kushiriki katika WIki ya Utumishi wa Umma 2014



Tume ya Ushindani ni moingoni mwa Taasisi, Idara za Serikali  Wakala na Wizara zitakazoshiriki katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2014.

Kurugenzi zote za Tume ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Kurugenzi ya Uendeshaji; Kurugenzi ya Tafiti za Kiuchumi, Ushawishi wa Ushindani na Miungano ya Kampuni; Kurugenzi ya Utekelezaji wa Sheria na Kurugenzi ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia na Utetezi wa Mlaji, zitawakilishwa katika maonesho hayo.

Katika maonesho hayo, Tume inatarajia kuonesha shughuli zake inazozifanya kwa mujibu wa sheria inazosimamia utekelezaji wake ambazo ni Sheria ya Ushindani (Namba 8 ya mwaka 2003) na Sheria ya Alama za Bidhaa ya mwaka 1963, kama ilivyorekebishwa.

Kwa upande wa Sheria ya Ushindani, Tume inatarajia kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ambavyo inashughulikia masuala ya mashauri au kesi zinazohusu ukiukwaji wa misingi na sheria ya ushindani, pamoja na masuala ya utetezi wa Mlaji.

Aidha, Tume itaelezea kuhusu mikakati ya udhibiti wa Bidhaa Bandia kupitia Sheria ya Alama za Bidhaa ya mwa a1963, iliyorekebishwa, ikiwa ni pamoja na misako mbalimbali inayofanywa na Tume katika kudhibiti bidhaa Bandia nchini, kaguzi za kila siku katika maingilio ya bidhaa, hususan bandari na bandari kavu zake.

Pamoj na hayo, tume pia imejipanga kusambaza vipeperushi mbalimbali vitakavyotoa elimu kwa umma kama vile Ijue Tume ya Ushindani, Jinsi ya Kutambua Bidhaa Bandia pamoja na kipeperushi cha Haki na Wajibu wa Mlaji.
Mbali ya Vipeperushi hivyo, Tume pia itatoa elimu kwa vitendo kuhusu jinsi ya kutambua bidhaa bandia kwa wananch watakaotembelea banda lake.

Utambuzi wa viashiria vya msingi vya bidhaa bandia ni suala muhimu kwa mlaji awapo sokoni kwa kuwa litasaidia kumuwezesha kutilia mashaka bidhaa husika na kuikagua zaidi kabla ya kufanya uamuzi wa kuinunua

Aidha, ili kujipanga katika kuboresha shughuli zake hapo baadaye, hususan katika eneo la utoaji elimu kwa umma, Tume inatarajia kuendesha zoezi la kukusanya maoni ya wananchi kuhusiana na namna wanavyopenda shughuli za Tume ziboreshwe na namna ambavyo kwa sasa wanakabiliana na changamoto mbalimbalil kimaisha zinazohusiana kwa namna fulani na shughuli za Tume; Mathalan, weledi na changamoto katika manunuzi ya bidhaa na huduma wawapo sokoni.

Banda la Tume ya Ushindani (FCC) lipo mstari wa kwanza, nyuma ya mabanda yaliyo mstari wa mbele unapoingia katika lango kuu la Viwanja vya Mnazi Mmoja. Banda lipo upande wa kulia ukiingia lango Kuu la viwanja hivyo.

Tunawakaribisha wadau wote kutembelea Banda la Tume ya Ushindani (FCC) Katika Maonesho ya WIki ya Utumishi wa Umma (2014) na kujifunza kuhusu shughuli za Tume. Katika banda hilo utaweza kupata maelezo mbalimbali kuhusu shughuli za FCC.